Muonekano wa jengo la Makumbusho ya Mkwawa


Ni kituo kilicho hifadhi historia ya mkoa wa Iringa, Historia ya wabantu (kabila la wahehe), zana za kivita, Fuvu la mtwa mkwawa, pamoja na vifaa vya kimila na desturi vilivyotumika katika maisha ya kila siku ya kabila la wahehe. Kituo hiki kinapatikana mkoa wa Iringa, kijiji cha kalenga umbali wa kilomita Kumi na mbili (12) kutoka Iringa Mjini.
Masimulizi ya Mtwa Mkwavinyika Munyigumba Mwamuyinga maarufu kama Chifu Mkwawa ni miongoni mwa masimulizi yenye kusisimua na kuteka hisia pindi uyasikilizapo, Kwa mujibu wa Mhifadhi malikale wa kituo hiki cha makumbusho ya Mkwawa Erick Jordan aliyetuelezea historia ya Mtwa Mkwawa anasema “Nipende kuwakaribisha sana katika Makumbusho ya Mkwawa ambayo yako chini ya Idara ya Malikale na kukasimishwa kwa Hifadhi za Taifa Tanzania (Tanzania National Parks), Mkwawa alizaliwa mnamo mwaka 1855 na kuaga dunia mwaka 1889 kwa kujipiga risasi katika eneo lijulikanalo kama Mlambalasi, mkwawa alipambana katika kupinga uvamizi wa kikoloni na kuwaua wanajeshi wa kijerumani mia tatu (300) na bwana mkubwa wao (Emil von zelewsky) A.K.A Nyundo."
Namna ya kufika
Makumbusho ya Mtwa mkwawa yapo umbali wa kilomita kumi na mbili (12) kutoka mji wa Iringa, yanafikika msimu wote wa mwaka, kwa njia ya baiskeli, pikipiki, bodaboda, gari N.K
Kwa maelezo na masimulizi Zaidi unakaribishwa kutembelea Makumbusho ya mkwawa yaliyopo Mkoani Iringa- Tumerithishwa, Tuwarithishe.
Follow us on:Twitter
Follow us on: Pinterest
Facebook acc: Uyole Cte
Blog: uyolecte.blogspot.com
Click Here to Follow us on Instagram
Facebook page: Uyole Cultural Tourism Enterprises
Comments
Post a Comment