Sehemu ya kuangaalizia Bonde la Ufa Mbeya, Tanzania

Muonekano wa bonde la usangu

 Muonekano wa barabara ya Chunya Mbeya uelekeapo Sehemu ya kuangalizia bonde la ufa
  
Kibao kilichopo kandokando ya barabara ya Chunya Mbeya kikionesha sehemu barabara iliyojuu Tanzania.

Mkoa wa Mbeya ni moja kati ya mikoa ya Tanzania inayopitiwa na Bonde la ufa ( Bonde la ufa Kuu) linalosadikika kutokea miaka thelathini na Tano (35) milioni iliyopita, bonde hili lina urefu wa Kilomita (Km) 6400 na Upana wa kilomita (Km) 64 likianzia Bara la Asia, Afrika Mashariki na mwisho Msumbiji.

Sayari ya Dunia hapo awali ilikuwa bara moja lililojulikana kama PANGEA Kutokana na mitikisiko ikajigawa ikasababaisha kutokea kwa Mabara saba ambayo ni Bara la Afrika, Bara la Asia, Bara la Amerika ya Kaskazini, Bara la Amerika ya Kusini, Bara la Antaktika, Bara la Ulaya, Bara la Australia. Hivyo tafiti za wanajigrafia zinaonyesha kuwa miaka kadhaa ijayo Nchi za Afrika mashariki (Kenya, Uganda na Tanzania) zitajigawa kutokea bara lingine

Bonde hili la ufa limejigawa katika sehemu kuu ambazo ni: Mkondo wa Mashariki, Mkondo wa Magharibi na mkondo wa Kusini.

Mkondo wa Mashariki, Mkondo huu unaanzia kuonekana katika nchi ya Syria (Magharibi mwa bara la Asia) kuelekea Kusini mpaka nyanda za juu za Ethiopia, Somalia kuja Kenya kupitia ziwa Turkana, Kwa Tanzania limepita ziwa Natron. lapanuka pasipokuonekan tena kwa macho Kwenye bonde la Usangu linaonekana kama bonde lenye safu za milima kando.

Mkondo wa Magharibi, huonekana vizuri kuanzia ziwa Albert na kuendelea katika maziwa ya ziwa Edward, ziwa Kivu, ziwa Tanganyika na ziwa Rukwa.

Mkondo wa Kusini, Bonde la ufa likianzia Katika bonde la usangu(ambapo mkondo wa mashariki na mkondo wa magharibi imekutana), linaendelea mpaka Ziwa Nyasa, halafu katika mabonde ya mto Shire na sehemu ya mwisho wa mto Zambezi hadi kuingia katika Bahari ya Hindi.

Mkoa wa Mbeya ni sehemu pekee ambapo pande zote za bonde la Ufa zinakutana (Mashariki, Magharibi na Kusini).

Pia unaweza kuliona kwa uzuri bonde hili kupitia maeneo mbalimbali ndani ya mkoa wa Mbeya, Lakini sehemu nzuri zaidi ni sehemu iitwayo VIEWING POINT ambayo inapatikana katika eneo la misitu ya Kawetile barabara ya kuelekea Chunya, eneo hili ni zuri haswa kwa muonekano wake, hali ya hewa mwanana na linamuwezesha mtembeleaji kuona bonde la ufa kwa muonekano mzuri zaidi..

Kwa mtalii Ukitokea Mbeya mjini kuelekea eneo hilo utaweza kuona vitu mbalimbali kama; eneo maalum kwaajiri ya kutizama muonekano wa jiji (MBEYA CITY VIEWING POINT), Barabara ya Uwanda wa Juu kuliko zote Tanzania (THE HIGHEST POINT OF ALL TRUNK ROADS IN TANZANIA), yenye Muinuko wa 2457M latitudo 0835'S longitudo 3325'E, Soko dogo la viungo (spice) na vyakula lililopo njiani, Kona kali sana iliyopewa jina la kona ya mkoa na mwisho kabisa ni sehemu ya kuangalizia bonde la ufa. Ambapo ukiwa sehemu hii utaweza kuona sehemu kubwa ya Bonde la usangu, ukiwa na kiona mbali (Darubini) unaweza kuona sehemu ya hifadhi ya Taifa ya Ruaha.

Kwa mawasiliano zaidi wasiliana nasi kupitia, 
Barua pepe: uyolecte@gmail.com 
Simu: +255783545464 
S.L.P 475 Uyole Mbeya.
Facebook: Uyole cultural tourism enterprise
Facebook: Uyole CTE 
Twitter: @uyolecte

Comments

  1. Uyole Cultural Tourism Enterprises: Sehemu Ya Kuangaalizia Bonde La Ufa Mbeya, Tanzania >>>>> Download Now

    >>>>> Download Full

    Uyole Cultural Tourism Enterprises: Sehemu Ya Kuangaalizia Bonde La Ufa Mbeya, Tanzania >>>>> Download LINK

    >>>>> Download Now

    Uyole Cultural Tourism Enterprises: Sehemu Ya Kuangaalizia Bonde La Ufa Mbeya, Tanzania >>>>> Download Full

    >>>>> Download LINK

    ReplyDelete

Post a Comment