MATUKIO: Mfululizo wa Matukio ya Wiki ya Utalii Mkoani Mbeya

Wadau wa Utalii wakiwa katika Viwanja vya Nane Nane




Wa Kwanza Kulia mkuu wa Wilaya Mbeya Rashidi Chuachua akipokea Maandamano ya wadau wa utalii katika eneo la Mnara wa Mashujaa



Wadau wa Utalii wakiwa Kisiba Campsite

Maporomoko ya Maji Kapologwe

Ndani ya Ukumbi wa Mkapa

Wiki ya Utalii Mkoani Mbeya iliadhimishwa kwa kuwa na mfululizo wa matukio mbalimbali kama ifuatavyo

Tarehe 21/09/2021 
Ziara katika vyombo vya habari ikiwemo Redio, Televisheni ilimkuhamasisha na kutoa elimu kwa wananchi juu ya umuhimu wa utalii

Tarehe 22/09/2021 
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Juma zuberi Homera alifanya press ya ufunguzi wa wiki ya Utalii Mkoani Mbeya. 

Tarehe 24/09/2021, Siku ya Ijumaa
Wadau wa utalii walifanya Road show kuanzia nane nane Mbeya mpaka Mnara wa mashujaa ambapo msafara huu ulipokelewa na mkuu wa Wilaya Mbeya Rashidi ChuaChua 

Tarehe 25/09/2021, Siku ya Jumamosi

Wadau kwa kushirikiana  na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa walifanya Safari ya kitalii kwenda KISIBA CAMPSITE, kabla ya kufika walitembelea Mti Mkubwa wa Katembo uliopo masoko ambao ili kuuzunguka unahitaji kwatu 12 wakiwa wameshikana mikono, na kisha baadae kuelekea Kisiba Campsite wapo wadau walirudi Mbeya lakini wapo wadau walifanya Camping

Tarehe 26/09/2021, Siku ya Jumapili

Asubuhi wadau waliamka na kufanya michezo mbalimbali na kisha kuelekea Maporomoko ya maji Kapologwe kisha kuelekea Mbeya. 

Tarehe 27/09/2021, Siku ya Jumatatu
Tulikutana katika ukumbi wa mkapa kwa ajili ya kufanya Tathimini ya wiki ya utalii

Shughuli hii ilipewa nguvu na UPL SAFARIS, EVERDAY MBEYA, KISIBA CAMPSITE, UTALII NA KALAMU, UTENGULE COFFEE LODGE, PHOENIX HOTEL, G TOWN HOTEL, HILL VIEW HOTEL, BUSOKELO TV NA BONGE GARAGE

BOFYA KUTAZAMA VIDEO









 

Comments