PANGO LA IBADA NKYALA (NKYALA RITUAL CAVE)

Wilaya ya KYELA ni wilaya mojawapo kati ya wilaya za mkoa wa mbeya. wilaya ya Kyela inapatikana kusini mwa mkoa wa Mbeya kandokando ya ziwa lenye sifa lukuki duniani ZIWA NYASA.

Wilaya ya kyela inapakana na nchi ya Malawi, ziwa nyasa, mkoa wa Iringa (wilaya ya makete), wilaya ya Ileje pamoja na wilaya ya Rungwe, leo tutaangazia macho yetu Nkyala ritual cave.


NKYALA ritual cave ni pango lipatikanalo wilaya ya kyela mkoani Mbeya Tanzania. Muonekano wa pango hili si pana sana bali ni refu sana, Inasemekana limetoka Matema kyela kwenye kingo za safu za milima livingstone, likipita chini kwa chini katika safu za milima livingstone mpaka Rudewa japo haijathibitishwa kitaalam, wapo popo ndani yake japo si wengi sana kama wale wanaopatikana SONGWE BAT CAVE, lakini pango hili kuna giza nene sana maana hakuna sehem mwanga unapenya.

Kutokana na giza nene ndani ya pango hili, uwapo wa popo, na hofu ya kukutana na viumbe vyenye kuhatarisha maisha yetu hatukuingia ndani sana, na hii ilisababishwa na mwenyeji wetu ambae alitusihi sana kutoingia na kadri tulivyokuwa twaingia alibaki nje na alionekana kuwa muoga sana.

Wenyeji wanasema pango hili lina umuhimu sana katika historia ya wakazi wa eneo hili inayotakiwa kutunzwa ili kuja kueleza vizazi vijavyo. Hapo kale lilitumika na viongozi wa kimila (machief wa eneo la matema) kama sehemu ya kuabudia Haya yanathibitishwa na uwepo wa chungu ndani ya pango hili ambacho kilitumika katika matambiko yao ya kimila. Lakini pia wanasema Ni sehemu ambayo zilikuwa zapatikana kuku zenye rangi nyeupe (kuku pori) tangu wazee waache kupatumia kwa ibada hata kuku wamepotea na hawaonekani tena.

Ili kuweza kufika sehemu hii ya kihistoria ni mpaka upande mtumbwi safari inayochukua dakika kadhaa mkitokea vijiji vya pembezoni (mwambao wa ziwa nyasa) mnapita sehemu ambayo hatuji isahau maan ilitubidi kumuomba muongoza mtumbwi asimame japo kwa dakika tushangae uumbaji wa Mungu tulipita makazi ya samaki wa rangi mbali mbali wakiwemo wa njano, bluu, nyeusi, mchanganyiko nyeupe na nyeusi (pundamilia) n.k Ziwa Nyasa linajulikana kuwa na aina nyingi za
samaki (zaidi ya 1500). Aina chache tu zinavuliwa kama chakula lakini aina mbalimbali zinakamatwa na kuuzwa nje ya Afrika kwa wapenzi wa samaki zenye rangi.

Kama unachochote wajua au uliwahi sikia juu ya pango hili karibu utuelimishe kupitia comments au fika ofisi zetu zilizopo uyole ya kati mkoani mbeya.

Kwa safari za kufika hapa wasiliana nasi 0783545464/0766422703
uyolecte@gmail.com

Comments