
NTOTOFULA ni neno la Kinyakyusa lenye maana ya Povu, Sehemu hii ya kuogelea inayopatikana ndani ya Mto Mbaka katika kijiji cha Mbambo Halmashauri ya Busokelo iliitwa hivyo kutokana na uwepo wa povu la asili litokanalo na maji kujipiga kwenye Mwamba/mawe ama ukuta wa asili. Eneo hili limekuwa likitumika kutoka kizazi hadi vizazi kwa shughuli za kuogelea kwa wakazi wa maeneo haya.
Uongozi
wa Gwankaja Farm lodge wameamua kufanya juhudi mbalimbali za kuongeza
thaman eneo hili ikiwemo kulitangaza ili liweze kutumiwa kwa shughuli za
kiutalii na michezo ikiwemo kuogelea ama kupunga upepo.
Gwankaja
Farm lodge ni sehemu inayopatikana umbali wa kilomita ishirini na saba
tu (27) kutoka tukuyu Mjini ambayo mgeni anaweza kupata huduma
mbalimbali kama vile kupiga kambi (Camping), Malazi, Chakula N.K, Hii
kuifanya sehemu hii kuwa muhimu sana kutokana na ukaribu wake kwenda
kwenye vivutio mbalimbali hasa vile vipatikanavyo Halmashauri ya Wilaya
ya Rungwe.
Credit: Mazplusfly | Photobank studio | Uyole cultural tourism enterprise
Book Your trip with us.
Follow us on:Twitter
Follow us on: Pinterest
Facebook acc: Uyole Cte
Blog: uyolecte.blogspot.com
Click Here to Follow us on Instagram
Facebook page: Uyole Cultural Tourism Enterprises
Comments
Post a Comment