RAS Njombe Atembelea Hifadhi Ya Taifa Kitulo

Katibu Tawala Mkoa Wa Njombe Bi Judica H Omari akiongozana na Katibu Tawala Msaidizi Sehemu ya Uchumi na Uzalishaji Ayoub Mndeme Pamoja Wakala wa Barabara Tanroads Mkoa wa Njombe.

Wamefanya ziara katika hifadhi ya Taifa ya Kitulo ikiwa na lengo la Kukagua miundombinu pamoja na kutangaza utalii wa ndani, amepongeza sana juhudi zinazofanywa na uongozi wa Hifadhi ya Taifa Kitulo kuimarisha uhifadhi, miundombinu na Kutangaza Vivutio Vya Utalii vipatikanavyo katika Hifadhi ya Taifa Kitulo.


Aidha Katibu Tawala wa mkoa wa Njombe Bi Judica Omari amemshukuru Raisi wa Jamhuru ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan kwa mambo mbalimbali ikiwa ni pamoja na uamuzi wa kuzindua mbio za mwenge katika mkoa wa Njombe wakati ambapo mkoa huo unaaadhimisha miaka Kumi (10) tangu kuanzishwa kwake mnamo mwaka 2012.

Wa kwanza Kushoto Ni Katibu Tawala Mkoa wa Njombe Bi Judica Omari, wa pili Katibu Tawala Msaidizi sehemu ya uchumi na uzalishaji Ayoub Mndeme, Mratibu Uyole cultural tourism enterprise na Mkurugenzi Kisiba Campsite Amos Asajile, Meneja Gwankaja Farm Lodge Daniel Mlamka na mwisho ni Adam Gwankaja Mkurugenzi Gwankaja Limited Akielezea dhima ya safari yao ndani ya Hifadhi ya Taifa Kitulo, kwa katibu tawala wa Mkoa wa Njombe waliyekutana nae ndani ya Hifadhi ya Taifa Kitulo.

Wa pili kushoto Kamishina Msaidizi wa uhifadhi Hifadhi ya Taifa Kitulo Theodora Aloyce, akitoa maelezo juu ya sehemu hii ya kuangalizia Muonekano wa Mashamba, vijiji vya Matamba na Kinyika, sehemu iliyomvutia Katibu Tawala Wa Mkoa Wa Njombe pamoja na Alioambatana Nao. 


Afisa Utalii Hifadhi ya Taifa Kitulo Susani Tesha Akionesha Muonekano wa Mashamba na Kijiji cha Matamba.


Picha & Video: Petro Damian(PetroDamian7), Zakaria Mgala(Mazplusfly), Exavery Mwakagali(Photobankstudio), Albert Chafu(Nyangumimedia).

Comments

Post a Comment