MKE WA ROMA MKATOLIKI ATEMBELEA VIVUTIO VYA KITALII MBEYA

Mwami Daniel Mkurugenzi Nancy Tours LTD Akiwa Kisiba Campsite

Sophia Azizi akiwa kwenye enao la Maporomoko ya Maji ya Kapologwe, Yapatikanayo Halmasahuri ya Wilaya ya Rungwe.


Mke wa Mwanamuziki maarufu wa Kizazi Kipya Nchini Tanzania Roma Mkatoliki, Mwami Daniel ambae ni Mkurugenzi wa Nancy Tours LTD Yenye makao Makuu yake Jijini Dar es Salaam.

Amefanya safari ya Kitalii mkoani Mbeya na kutembelea Vivutio mbalimbali kwa lengo kutangaza vivutio vya kitalii vilivyopo mkoani Mbeya, baadhi ya vivutio alivyoweza kuvitembelea ni pamoja na Maporomoko ya Maji  Kapologwe, Mlima wa tatu kwa urefu Nchini Tanzania Mlima Rungwe, Maporomoko ya Maji Malamba, Daraja la Mungu Kiwila, Kisiba Campsite, Sehemu ta Kuangalizia Bonde la Ufa na Kijungu Jiko

Akiwa wilayani Rungwe alipokelewa na Kaimu Mkurugenzi wa Wilaya ya Rungwe Castory Makeula pamoja na Afisa Utalii wa Wilaya ya Rungwe Numwagile Bughali, Afisa Habari wa Wilaya ya Rungwe Noah Kibona, katika mapokezi haya Kaimu Mkurugenzi alitumia nafasi hii kuelezea Vivutio vya kitalii vilivyopo Halmashauri ya Wilaya ya Rungwe pamoja na Shughuli mbalimbali ambazo Mgeni ama mtalii atembeleapo Wilaya ya Rungwe anaweza Kuzifanya.

Mkurugenzi wa Nancy Tours LTD Amevutiwa sana na vivutio vya kitalii vipatikanavyo mkoa wa Mbeya hususani Wilaya ya Rungwe na ameahidi kuuunga mkono juhudi za serikali katika kutangaza utalii ili kukuza sekta ya Utalii Nchini, “Nianze kwa kutoa shukrani za dhati kwa uongozi wa Halmashauri ya wilaya ya Rungwe kwa mapokezi yao, pia nitoe pongezi kwa juhudi mbalimbali wanazofanya katika kutangaza vivutio vya vya kitalii vipatikanavyo Wilaya Ya Rungwe

Nimetembelea vivutio mbalimbali vya kitalii nchini lakini katika mikoa tofauti, Lakini mkoa wa Mbeya unavivutio vya kipekee na vyenye kuvutia sana, ninaunga mkono juhudi za serikali katika kutangaza vivutio vya kitalii pamoja na fursa za kiuwekezaji, nitumie fursa hii kuwakaribisha watanzania wenzangu na wageni kutoka Nje ya Tanzania kuweza kutembelea vivutio hivi vya kitalii vilivyopo Mkoani Mbeya” 

Aliongeza kwa kusema amefanya ziara hiyo ili kuongeza hamasa na kuchochea hali ya utalii wa Ndani kwa watanzania, Nitumie fursa hii kumshukuru Mkurugenzi mtendaji wa Wilaya ya Rungwe Bwana Renatus Mchau kwa mchango wake mkubwa katika kufanikisha zoezi hili, Ameyasema haya alipokuwa akiongea Mbele ya viongozi waliompokea Halmashauri ya Wilaya ya Rungwe. 

Karibu Mbeya, Karibu Tanzania.

Book Your trip with us.
Email: uyolecte@gmail.com
Whatsap/ Sms/ Call +255 783 545 464

Follow us on:Twitter
Follow us on: Pinterest
Facebook acc: Uyole Cte
Blog: uyolecte.blogspot.com
Website: www.uyolecultural.com
Click Here to Follow us on Instagram
Facebook page: Uyole Cultural Tourism Enterprises

Things to do in Mbeya | Mbeya tourist atractions | Uyole cultural tourism enterprise 

Comments