
Uongozi wa Jarida la Mbeya Advertise with Macrine mnamo tarehe 26/06.2021 ulizinda Jarida la utalii katika ukumbi wa Usungilo
Hotel Uliopo Mbeya Mjini.
Siku ya utalii na Kalamu uliambatana na uzinduzi wa
Kampeni ya utalii itakayogusa vijana wa shule wenye ari chanya katika ukuaji wa
utalii, Pamoja na Jarida la kutangaza Fursa mbalimbali nchini Tanzania.
Hafla hii ya uzinduzi ilihudhuliwa na wadau mbalimbali wa utalii katika ukanda wa Nyanda za Juu kusini mwa Tanzania, Baadhi ya wadau hao ni Bodi ya Utalii ofisi ya kanda iringa, Mamlaka ya wanyama pori Tanzania TAWA, Hifadhi ya Taifa Kitulo, pamoja na wadau mbalimbali kutoka ndani na nje ya mkoa wa Mbeya.
mnamo juni mwaka 2018 tulifanikiwa kuzindua jarida
letu la utalii lililokuwa limejikita zaidi kuibua fursa na kutangaza utalii wa
Nyanda za juu Kusini mwa Tanzania, baada ya kufanya utafiti na kutambua fursa
mbalimbali zilizopo katika nchi yetu, uongozi wa jarida umeamua kupanua wigo wa
matangazo katika fursa mbalimbali za utalii, uwekezaji na biashara Kutoka
nyanda za juu Kusini na kuwa Tanzania Nzima. Kwa sasa jarida hili litajulikana
kama M MAGAZINE, Jarida hili
linategema kusambazwa kama FREE MAGAZINE kwenye
ofisi mbalimbali za uma na taasisi binafsi "alieleza Bi Macrine Ntabagi"
Akaongeza kwa kusema Pamoja na mafanikio makubwa
katika kuwafikia watanzania wengi, uongozi umeamua kuwa na kampeni rasmi
inayoitwa UTALII NA KALAMU, tukiwa
na maana utalii unaongezwa ubunifu na kuenzi maandishi, katika kampeni hii
tutakuwa na mijadala mbalimbali, CLUB za utalii, na mashindano kwa wanafunzi
ili kupata wanafunzi wwenye uelewa katika masuala ya utalii watakao kuwa
mabalozi wazuri wa utalii kwa siku za mbeleni.
Dr Anjelina Lutambi akijibu lisala iliyosomwa na Mkurugenzi wa Utalii Bi Macrine, alisisitiza ushirikiano baina ya wadau, kutafuta eneo ambalo itaweza kuwekwa information centre itakayoweza kurahisisha upatikanaji wa taarifa za utalii, lakini pia kutoa ushirikiano kwa wadau wote wa utalii, kukaa pampoja na wadau pamoja na kurudisha kamati za utalii za wilaya na Mkoa, akizungumza kuhusu miundombinu alisema Ofisi imejipanga na kuahidi kwamba suala la Miundombinu si muda mrefu itabaki historia.
Comments
Post a Comment