Maporomoko ya Maji Nyaugenge/ Nyaugenge Waterfalls

Muonekano wa Maporomoko ya Maji Nyaugenge



Maporomoko ya Maji Nyaugenge Yanapatikana ndani ya Pori la Akiba La Mpanga Kipengele linalosimamiwa na Mamlaka ya usimamizi wanyama Pori Tanzania (TAWA, Pori la Mpanga Kipengere linapatikana nyanda za Juu Kusini mwa Tanzania katika Mkoani Mbeya Wilaya ya Mbarali, na Mkoa wa Njombe Wilaya ya Wanging’ombe na Makete.

Kwa Mujibu wa Askari wa TAWA Leonard Nsajigwa anasema "Nyaugenge Ni neno la Kabila la wawanji lenye maana ya Gema (Kiswahili)" Maporomoko haya yako Umbali wa Kilomita Moja (1) Kusini Mashariki mwa Maporomoko ya Maji Kimani.

Mara baada ya kushuka kwenye gari katika sehemu maalum ya kuegesha gari unakaribishwa na sauti kuu ya maanguko ya maji ya Kimani, ukisogea mbele kidogo unaanza kuyaona maporomoko haya kupitia uwazi wa kwenye miti. Ukishuka ngazi ndipo utaona barabara ielekeayo Katika Maporomoko ya Maji ya Nyaugenge.

Mandhari ya maporomoko haya ni ya pekee sana, kwanza yamezungukwa na Miamba yenye mvuto sana, Ukitizama picha mara baada ya anguko dogo la kwanza maji yamepita chini kwa chini na kisha kufanya anguko la pili.

Kiujumla uzuri huu si wa kusimuliwa, unaweza kufanya safari yako kisha ukajionea uzuri huu nawe ukaweza kuwasimulia wengine.

Photo Credit & Drone Operations: Mazplusfly

Photo Credit & Video:Photo Bank Studios 

Makala & Guiding: Chikanda safaris & adventure

MediaBusokelo Tv (Subscribe Busokelo Tv, ili usipitwe na habari moto moto za utalii na utamaduni pamoja na habari Zinginezo)


Karibu Mbeya | Karibu Tanzania

Help us to share with your friends, For more tourism updates follow us on the following social networks

Things to do in Mbeya | Mbeya tourist atractions | chikanda safaris & adventure

Comments