Muonekano wa Maporomoko ya Maji Kimani
Siku ya Ijumaa Tarehe 05/06/2021 Tulifanya safari ya kutembelea pori la akiba la Mpanga Kipengere na kupiga kambi tukitokea Mkoani Mbeya. katika safari hii tuliambatana na Mazplusfly, Photo Bank studios Pamoja na Busokelo Tv
Pori la Akiba la Mpanga/Kipengele linapatikana nyanda
za Juu Kusini mwa Tanzania katika Mkoani Mbeya Wilaya ya Mbarali, na Mkoa wa Njombe
Wilaya ya Wanging’ombe na Makete. Pori Lina ukubwa wa Kilomita za Mraba 1574
kwenye mwinuko wa mita 1300 – 3000 kutoka usawa wa Bahari. Pori hili linasimamiwa na Mamlaka ya usimamizi wanyama Pori Tanzania (TAWA)
Maporomoko ya Maji Kimani yanapatikana ndani ya Pori
la Akiba la Mpanga/Kipengere umbali wa Kilomita kumi na tatu (13) Kutoka Barabara
Kuu ya Mbeya – Iringa, muonekano wa maporomoko haya unavutia sana kutokana na
namna maji haya yanavyo anguka katika mwamba wenye ngazi ngazi pamoja na uwepo
wa sehemu za kuogelea. Unaweza kufanya utalii wa kupanda miamba (Rock
climbing), Kuogelea (Swimming), kupiga picha (Video & Photo Graphing) N.K
Vivutio vingine Vipatikanavyo katika Pori la Akiba la Mpanga Kipengere ni Pamoja na
1. Maporomoko ya Maji saba (7) ambayo ni Kimani, Nyaugenge, Lyamakonokwila, ikovo, Kipengere, merere, na Allan
2. Pango
La Chifu Mkwawa, lililopo Karibu kabisa na maporomoko ya maji ya Kimani, Ambalo
lilitumika kama sehemu ya maficho ya Chifu Mkwavinyika Munyigumba Mwamuyinga
(Mkwawa) kiongozi wa kabila la Wahehe.
3. Bafu
la Chifu Mkwawa, lililopo katika Mto Kimani mita chache Kutoka lilipo pango la
Chifu Mkwawa, Bafu lina ngazi mbili alizokuwa akizitumia kushuka na kupanda.
4. Kisugulio,
Jiwe alilolitumia chifu Mkwawa
5. Mabaki
ya Mafiga, Yapo Mawe Matatu yanayofanya Mafiga yaliyotumika kuchoma na kupikia
vyakula.
6. Jiwe
la Kusagia, jiwe hili lilitumika na chifu mkwawa kusagia nafaka ikiwemo Uwele,
Mtama, Chumvi/Magadi, Vyakula na dawa za Mizizi.
7. Fuvu La Nyani, aina ya Yellow Baboon Lililohifadhiwa
ndani ya pango la Chifu Mkwawa.
8. Zana
za Kale zilizotumika na Chifu Mkwawa.
9. Mkusanyiko
wa Mawe ya Kubisha hodi
10.Uoto
wa Asili. Wenye miti aina ya Miombo
11.Kipembo,
neno la kiwanji lenye maana ya “Jivu” ni eneo la Njia ya watumwa lililotumika
kuwachoma moto watumwa waliokuwa wamechoka na wagonjwa.
12.Aina
mbalimbali za miamba
13.Ukanda
wa Maua ya Asili aina ya (Orchid) katika eneo la Ibaga
Shukrani za dhati kwa uongozi wa TAWA kwa mapokezi, Huduma na ushirikiano mkubwa tulioupata Ambrosy Mng’ongo Kamishna msaidizi mwandamizi TAWA, Joas Makwati Meneja Mpanga Kipengere na Leonard Nsajigwa Askari Muongoza Watalii
Photo Credit & Drone Operations: Mazplusfly
Photo Credit & Video:Photo Bank Studios
Makala & Guiding: Chikanda safaris & Adventure
Media: Busokelo Tv (Subscribe Busokelo Tv, ili usipitwe na habari moto moto za utalii na utamaduni pamoja na habari Zinginezo)
Things to do in Mbeya | Mbeya tourist atractions | Chikanda safaris & Adventure
Comments
Post a Comment