Miaka mitatu (3) ya usiku wa maharusi (The great Rift Valley Viewing Point)

 







Usiku wa maharusi kwa kushirikiana na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mbeya waliandaa safari ya kitalii kuelekea sehemu ya kuangalizia Bonde la ufa (Viewing Point) Usiku wa Maharusi ni miongoni mwa matukio yanayoandaliwa na Kuratibiwa na Mc Edwin Luvanda, Leo tarehe 24/04/2020 ilikuwa ni maadhimisho ya miaka mitatu (3) ya tukio la usiku wa maharusi.

Katika ufunguzi wa safari hii Mkuu wa wilaya ya Mbeya Wiliam Ntinika ameelezea utajiri mkubwa sana uliopo mikoa ya Nyanda za juu kusini  katika sekta ya utalii kwa kutaja baadhi ya vivutio vya utalii ikiwemo, Hifadhi ya Taifa ya Ruaha, Hifadhi ya Taifa ya Kitulo, Kimondo cha Mbozi, Ziwa Ngosi, Ziwa Kisiba, pamoja na Fukwe za ziwa Nyasa. Pia akaeleza mipango ya mkoa katika kuongeza idadi ya watalii.

Mara baada ya kufungua Maadhimisho haya, msafara ulielekea moja kwa moja Kawetele yalipokuwa Mageleza ya zamani, kisha kuelekea Sehemu ya kuangalizia Bonde la ufa.

Katika Eneo la Bonde la ufa shughuri mbalimbali ziliweza kufanyika ikiwemo michezo ya Drift ilyofanyika na Mbeya racing Community, Kuvuta Kamba pamoja na burudani Mbalimbali

Maadhimisho haya yamepewa nguvu na wadau Mbalimbali wakiwemo Tigo, Ally Rich sanaa, Newforce, Mc Danny Fm, Alvin Desgn, Kisiba Campsite, Upl Safaris N.K

Photo Credit: Mazplusfly
Makala: Uyole cultural tourism enterprise

Karibu Mbeya | Karibu Tanzania


Help us to share with your friends, For more tourism updates follow us on the following social networks
Follow us on:Twitter
Follow us on: Pinterest
Facebook acc: Uyole Cte
Blog: uyolecte.blogspot.com
Website: www.uyolecultural.com
Click Here to Follow us on Instagram
Facebook page: Uyole Cultural Tourism Enterprises

Things to do in Mbeya | Mbeya tourist atractions | Uyole cultural tourism enterprise  

Comments

  1. It is a welcome alternative Tourism Spot from the 'overtrodden' Northern Circuit Destinations

    ReplyDelete
  2. You are most welcome, kwa habari zaidi unaweza kutufollow kwenye mitandao yetu ya kijamii kwa jina la Uyole cultural tourism

    ReplyDelete

Post a Comment