Ziwa Kyungululu llinapatikana Lugombo katika kijiji cha Kabembe kata ya Itete,
Halmashauri ya Busokelo Wilaya ya Rungwe, linapatikana umbali mdogo kutoka ilipo
Hospitali teule ya Itete.
Uwapo katika eneo lilipo Ziwa Kyungululu utaweza kuona kwa uzuri Mlima Sutwa,Safu
za Mlima Livingstone iliyoambaa mpaka katika Kingo za Ziwa Nyasa, pamoja na
ziwa Nyasa, Katika ziwa hili Hakuna mto wowote unaoingiza wala kutoa maji unaoweza
kuonekana kwa macho
Zipo Nadharia Mbalimbali juu ya utokeaji wa Ziwa Kyungululu japo tutajikita
zaidi katika nadharia mbili Moja ikiwa ni masimulizi ya wazee na Mbili kutokana
na Sayansi/Jiografia.
Katika masimulizi ya kihistoria juu
ya utokeaji wa ziwa Kyungululu tulipozungumza na wazee kila mmoja alisimulia
kwa namna yake lakini asilimia Kubwa walilenga kitu kimoja.
“kulikuwa na mtu mmoja alitoka sehemu za mbali sana na kufika mahali hapa,
alipofika alionekana kuwa ovyo sana kwa maana ya kwamba alikuwa mchovu na
mchafu sana mithiri ya mtu aliyegalagazwa katika vumbi na mchovu kana kwamba alitembea
umbali mrefu sana, aliingia katika nyumba ya kwanza ili kuomba maji ya kunywa
kutokana na hali aliyokuwa nayo ya uchafu walimkatalia, basi akasogea katika
nyumba ya pili vivyo hivyo wakamkatalia na kumfukuza.
Alipofika katika nyumba ya tatu alimkuta mama mmoja msamalia mwema ambae
alimuonea huruma kwa hali aliyokuwa nayo na kumkirimu kwa kumpa maji ya kuoga,
akamvisha nguo zingine na kisha kumwandalia chakula, mara baada ya kumaliza
kula ndipo yule mtu akamwambia mama yule uhame mahala hapa uhamie sehemu
nyingine kwa maana hapa patatokea maajabu.
wale watu walipomwona mama yule
anahama wakamsema na kumtukana kwa kusema kichaa anamhamisha na kumuona kama
mtu asiekuwa na akili kabisa, baada ya kutii agizo lile ikawa kama pigo kwa
wale watu pamoja na kijiji kwa ujumla pahala pale Pakadidimia na kisha
yakaibuka maji na kufanya sehemu ya Ziwa tunaloliona hivi leo.
Masimulizi hayo yalitumika ili kutoa elimu kizazi hata kizazi kuzifanya jamii
kuwa na ukarimu na upendo maana masimulizi hayo hayo yalitumika
hata katika maeneo mengine mfano kisiba, ikapu, ilamba na Kingili.”
Kwa Mujibu wa Nadharia ya KItaalam (Sayansi/Jiografia) Inaelezwa Kwamba Ziwa
Hili lilitokana na Milipuko ya Kivolkeno iliyotokea Miaka Mingi iliyopita,
Katika maeneo ya karibu Maziwa Mengine yaliyotokana na Milipuko ya Kivolkeno ni
Pamoja na Ziwa Ngosi, Ziwa Kisiba, Ziwa Ilamba, Ziwa Itende, Ziwa Ikapu pamoja
na Ziwa Kingili
Kwa safari za kitalii/ habari za utalii na
utamaduni katika mkoa wa Mbeya karibu UYOLE CULTURAL TOURISM ENTETPRISE.
Project: Karibu Southern Circuit Program
Photo Credit: Mazplusfly (Zakaria Mgala)
Book Your trip with us.
Email: uyolecte@gmail.com
+255 783 545 464
Follow us on:Twitter
Follow us on: Pinterest
Facebook acc: Uyole Cte
Blog: uyolecte.blogspot.com
Website: www.uyolecultural.com
Click Here to Follow us on Instagram
Facebook page: Uyole Cultural Tourism Enterprises
Things to do in Mbeya | Mbeya tourist atractions | Uyole cultural tourism enterprise
Comments
Post a Comment