Maporomoko ya Maji Kimani/ Kimani Waterfalls

Watalii wa ndani wakifurahia muonekano mzuri wa Maporomoko ya Maji Kimani

Muonekano wa Maporomoko ya Maji ya Kimani




Safari ya  Kitalii kutoka mbeya hadi Katika Pori la akiba la Mpanga Kipengele iliyoandaliwa na Mafioso ikijumuisha watalii Mbalimbali kutoka katika mikoa ya Nyanda za juu kusini mwa Tanzania.

Katika safari Hii ambayo waongoza watalii walikuwa ni Amos Asajile Kutoka Uyole Cultural Tourism Enterprise na Boyd Abuu kutoka Mafioso Tours waliweza kutoa maelezo mbalimbali pindi walipokuwepo safarini Mpaka tunafika katika Maporomoko ya Maji ya Kimani.

Maporomoko ya Maji ya Kimani ni miongoni mwa vivutio vya kitalii vyenye mvuto wa kipekee sana kutoka nyanda za juu kusini mwa Tanzania, Maporomoko haya yanawavutia watalii wengi sana kutokana na muonekano wake wa kipekee unaotiririsha maji kati ngazi ngazi na kisha kujimwaga sehemu ya chini na kufanya eneo lenye muonekano wa bwawa ambalo baadhi ya watalii huogelea.

Katika pori hili la akiba la mpanga kipengele pia yanapatikana maporomoko mengine ya Nyaugenge, lakini pia linapatikana pango ambalo inasemekana alikuwa akijificha Chifu wa Wahehe Mkwawa wakati wa Vita na Mjerumani, sio hivyo tu bali na mandhari nzuri zinazopendeza sana.

Katika Msimu huu wa sikukuu za Krismasi na Mwaka Mpya tunapenda kuwakaribisha wadau mbalimbali kuweza kutembelea vivutio vya kitalii vinavyopatikana katika mikoa na maeneo waliyopo.

Book Your trip with us.
Email: uyolecte@gmail.com
+255 783 545 464

Follow us on:Twitter
Follow us on: Pinterest
Facebook acc: Uyole Cte
Blog: uyolecte.blogspot.com
Website: www.uyolecultural.com
Click Here to Follow us on Instagram
Facebook page: Uyole Cultural Tourism Enterprises

Things to do in Mbeya | Mbeya tourist atractions | Uyole cultural tourism enterprise 

Comments