SIKU YA WANGONI Hufanyika Tarehe 26 Mwezi wa Pili na Ni siku ya kumbukumbu ya kihistoria kwa kabila la wangoni wote Afrika, Siku hii uadhimishwa kila ifikapo mwezi wa pili ikiambatana na maadhimisho ya kumbukumbu ya vita ya majimaji vilivyotokea miaka ya 1905-1907.
Siku hii muhimu inafanyika katika Kijiji cha Maposeni ambapo ndipo makao makuu ya chifu wa hapo zamani na hivi sasa anayejulikana kama Chifu Emanuel Zulu,
Gabriel Shawa Mkurugenzi wa UPL Safaris anasema Ikumbukwe VITA YA MAJIMAJI ilianza mwaka 1905-1907 na ilianzia katika Kijiji cha Maposeni, ambapo wanakijiji walikuwa wakiabudu na kufuata Mila zao chini ya Chief wao hivyo kutokwenda kujumuika Kuabudu katika misa zinazoendeshwa na na Padri FRASISCUS hali iliyipelekea kuamua Kulichoma jumba Au kwakingoni Mahoka ya chifu yaliyokuwa katika Kijiji cha MAPOSENI ambapo ndiyo makao makuu ya CHIFU Mputa Gwazelapasi Gama Hali iliyopelekea chuki kumkasirisha sana chifu wa eneo lile.
Kabila la Wangoni linahistoria pana sana pamoja na Mila na Desturi zake, Katika siku hii ya wangoni iinayojumuisha wangoni wote wapatikanao Afrika, utapata kuyafahamu mambo mengi sana na kujionea vitu mbalimbali ikiwemo Ngoma za Asili, Vyakula Vya Asili NK, Tupende kutumia Fursa Hii kukukaribisha mkoani Ruvuma katika NGONI TRADITIONAL FESTIVAL
NGONI TRADITIONAL FESTIVAL, Imeamdaliwa na UPL Safaris, Baraza la Makumbusho ya MajiMaji, Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Ruvuma Kwa kushirikiana na JWTZ, Itakayoanza Tarehe 25 mwezi wa pili na kuhitimishwa Tarehe 27 Mwezi wa Pili Kwa Mawasiliano zaidi ili kuweza kushiriki piga simu namba 0767 77 32 32 au 0767 26 61 34.
Katika sikuu hii ya Wangoni wageni wote ama washiriki wote watapata bahati ya kutembelea vivutio Mbalimbali vya mkoa wa Ruvuma ikiwemo Makumbusho ya Vita vya MajiMaji na vingine vingi.
Karibu Ngoni Traditional Festival.....
Comments
Post a Comment