Historia
ya mkoa wa Mbeya imegawanyika katika vipindi tofauti tofauti kabla ya uhuru na
baada ya uhuru, Mji wa Mbeya ulianzishwa na wakoloni waingereza mnamo mwaka
1927, Wakati huo dhahabu ilianza kupatikana
sana katika milima iliyopo karibu na Mbeya hadi Chunya hivyo Mbeya ulikuwa ni
mji wa mapumziko kwa Wazungu kutokana na hali yake nzuri ya hewa.
katika
kipindi cha ukoloni ulifahamika kama "Southern highland provience" kwa kujumuisha baadhi ya maeneo ya mikoa ya Iringa na
Rukwa na baadaye Mbeya. Asili ya neno Mbeya
imekuwa na nadharia kadha wa kadha ambazo zinaelezwa na wataalam na wazee
mbalimbali, Baadhi ya nadharia hizo ni pamoja na:-
1.
Ibheya - Chumvi
Nadharia
hii inaeleza kuwa asili ya Neno Mbeya ni neno la kisafwa "Ibheya" lenye
maana ya chumvi, Hii inatokana wafanyabiashara kufika katika mji huu na
kubadirishana mazao yao kwa chumvi iliyokuwa ikipatikana kwa wingi kipindi
hicho. Ikapeleka wenyeji kuita eneo hili Ibheya kama sehemu ya kubadilishia
chumvi na mazao, kutokana na sababu za kimatamshi ikapelekea wageni kuzoea
kutamka na kuandika Ibheya.
2.
Agamba mbeye - Kamlima Mbeye
Nadharia
hii inaeleza kuwa jina Mbeya limetokana na Mlima uliopo nyuma ya Chuo cha
Kilimo Uyole (Agricultural Research Institute -ARI- Uyole) uliojulikana kwa
jina la kisafwa kama Agamba Mbeye (kamlima Mbeye kwa kiswahili) Ambao hivi sasa
ni maarufu sana kwa jina la Mlima ugari, ni mlima ambao una muonekano wa
mviringo, sehemu za chini umeota nyasi japo si nyingi sana kama ilivyo sehemu
ya juu ambayo haioti nyasi kabisa, hivyo ikawa sehemu nzuri ya kupumzikia
wageni ili kupata hewa nzuri na muonekano mzuri wa mji, kutokana na changamoto
za kimataishi ikapelekea wageni kuliendeleza sana jina la eneo kama Mbeya
kimaandishi na kimatamshi.
Tunaendelea kukusanya taarifa za kuboresha makala hii, ukiwa na mawazo yoyote yenye kuboresha usisite kutuandikia katika mitandao yetu.
For more details and booking please contact us via.
Email: info@uyoleculturaltourism.com
uyolecte@gmail.com
Phone: +255783545464
P. O. Box 475 Uyole Mbeya.
Website: www.uyoleculturaltourism.com
Facebook: Uyole cultural tourism enterprise
Facebook: Uyole CTE
Instagram: @uyoleculturaltourismenterprise
Twitter: @uyolecte
Comments
Post a Comment