MKUU WA WILAYA YA CHUNYA MHESHIMIWA REHEMA MADUSA, APONGEZA JUHUDU ZINAZOFANYWA NA UYOLE CULTURAL TOURISM ENTERPRISES KWA KUSHIRIKIANA NA ELIMISHA NA CHAMA CHA BAISKELI KATIKA KUTANGAZA UTALII NA MCHEZO WA BAISKELI.

Mtunza hazina wa Chama cha Baiskeli Lukas Mhagama ambae ndiye likuwa kiongozi wa msafara huu, akizungumza mbele ya Viongozi wa wilaya Kushoto ni Mratibu wa Uyole cultural tourism enterprises Amos Asajile Mwamugobole, Lukas Mhagama mtunza hazina wa chama cha baiskeli, Mheshimiwa mkuu wa wilaya ya chunya Rehema Madusa, Afisa utamaduni Hope Musa, afisa Michezo Robert Mfugale.












Aliyasema haya alipokutana na uongozi wa Uyole cultural tourism enterprises, chama cha baiskeli mkoa wa Mbeya, Elimisha, wachezaji wa mchezo wa baiskeli pamoja na wadau tuliokuwa tumeongozana nao katika ukumbi wa Halmashauri. Awali alipongeza juhudi hizi huku akisema chunya ni sehemu nzuri sana ambayo inawachezaji wengi na wazuri ambao tutaweza kuwapata, lakini pia akaelezea suala la utalii akisema chunya ina vivutio vingi sana na wanampango wa kufungua jumba la makumbusho hivyo itasaidia kutunza kumbukumbu mbalimbali za kihistoria.

Lakini pia mkuu wa wilaya aliongozana na Afisa utamaduni Hope Mussa na Afisa Michezo Robert Mfugale ambao tunawashukuru kwa mapokezi yao mazuri, Walipozungumza kila mmoja kwa nafasi yake waliahidi kushirikiana nasi ili kuweza kutimiza malengo ya safari yetu.

Kwa sasa tunajiandaa na safari ya pili ambayo wachezaji watakimbia kwa baiskeli umbali wa KM 120 kutoka Mbeya kwenda kyela, tutalala na kesho yake tutaanza safari ya kurudi Mbeya hivyo kufanya jumla ya KM 240. Tunawakaribisha wadau kuja kujiunga ili kushiriki safari ijayo.

Comments