MALEMA/ KILAMBO VIEWING AREA

Viewing Area ni sehemu maalum ambayo hutengwa kwa ajili ya watu kuweza kutizama na kuona vitu mbalimbali ambavyo vinaweza kuwa umbali Fulani kwa upande wa bondeni na baadhi ya milima na miinuko mirefu, Hivyo basi ikawa ngumu kuona vizuri uwapo maeneo ya Malema/ Kilambo kuna sehemu nzuri ambayo yafaa ikatengwa kwa ajili ya kufanyika kuwa viewing area kama ilivyo katika ile barabara ya chunya (Kawetele).

Eneo hili ni zuri zaidi ki muonekano pia kwa shughuli za kitalii ambapo mtalii anaweza kuliona kwa ukubwa eneo ambalo imewahi kuwa mbuga ya wanyama kulingana na historia, muonekano wa Ziwa Kingili, Ziwa Ikapu, Sehemu za Ziwa Nyasa, Safu za milima Livingstone N.K, pia uoto wake wa asili unaovutia hivyo watalii wanaweza kufaidika mambo mengi ikiwepo hiyo ya kuyaona maeneo mengi kama tulivo yaainisha hapo juu.


Contact us:
Phone: 0756929868/ 0625747086
Email: uyolecte@gmail.com
instagram: uyoleculturaltourismenterprise
Facebook page: Uyole Cultural Tourism Enterprises
Facebook acc: Uyole Cte
Blog: uyolecte.blogspot.com
Visit our office Located at Uyole ya Kati Mbeya.

Comments