Sehemu iliyo hifadhiwa kwa kigezo cha kuhifadhi kumbukumbu ya zama za mawe na nguzo za miamba zilizotokana na mmomonyoko wa ardhi. Katika eneo hilo linalopatikana nje kidogo ya mji wa Iringa utaweza kujifunza historia ya zama za mawe zilizotumiwa na binadamu wa kale; zana hizo ni kama visu, kombeo, nyundo, sindano, mikuki, shoka n.k.
utaweza kujifunza historia na tamadu za makabila yanayo patikana mkoa wa Iringa Tena katika eneo hilo utaweza kujifunza na kutembelea eneo linalo badilika kwa muonekano kutokana na madiliko ya tabia ya nchi au mmomonyoko wa ardhi unaoonekana kama korongo linaloambatana na sehem ya udongo iliyobaki nakutengeneza nguzo ndefu za udongo na muonekano mionekano mingine tofauti tofauti.
Eneo hilo inasadikika kuwa miaka mingi iliyopita palikuwa na mkusanyiko wa maji pamoja na uwepo wa wanyama. Hivyo basi Ismila ni kati ya maeneo yanayo hifadhiwa ilikutunza historia za kitamaduni na asili (cultural and natural history) kama ilivyo Olduvai gorge
Comments
Post a Comment