GANGILONGA IRINGA, TANZANIA







Gangilonga ni neno la Kihehe lenye Nomino ambatani, neon hilo linatokana na maneno mawili ya kihehe ambayo ni iligangalyelilonga liganga lina maana ya jiwe lilonga likimaanisha lisemalo. Hivyo maana ya jiwe hili ni jiwe linalosema

Kuna maelezo ya aina mbili kuhusu tafsiri ya neon hili, moja inasema mwamba huu ulitumiwa na wahehe kama mahali pa matambiko na kuongea na mizimu, nyingine inaeleza kuwa wakati wa vita vya msituni kati ya mwaka 1894 hadi 1898 chifu mkwawa aliona Gangilonga kuwa mahali panapofaa nyendo na shughuli za wajerumani Iringa mjini. Maaskari wa Mkwawa waliigiza milio ya ndege kwa lengo la kupeleka taarifa muhimu kutoka sehemu moja hadi nyingine kwa umbali mrefu.

Lakini pia katika jiwe hili panaweza kutumiwa kama viewing area ya kuona sehemu kubwa ya iringa mjini, na idadi kubwa ya wageni hupendelea mida ya jioni kuangalia Sun set.

Comments