MASIMULIZI YA KALE/ STORRY TELLING



Uongozi wa UYOLE CULTURAL TOURISM ENTERPRISES kwa kushirikiana na ENVICULTURE (KYELA EMVIROCARE & CULTURAL TOURISM) unapenda kuwakaribisha wakazi wa Mkoa wa Mbeya siku ya Tarehe 8/ 10/ 2016 kutakuwa na masimulizi mbalimbali ya kale kutoka kwa wazee wetu wa zamani, ikiwemo Historia mbalimbali mfano Historia ya kabila la wanyakyusa, Tamaduni zao, na maisha yao ya kila siku. Hakuna mchango wowote ni kufika kwako kwenye uwanja wa Mzee Newton Mwakabambo Wilayani kyela karibu na dispensary ya Mkombozi.

Ambapo mshiriki atapata bahati ya Kuburudika kupitia Tanzu kama hadithi, ushairi, semi (methali, vitendawili, nk.).
Kuelimisha, kujua thamani za kijamii, historia yao, utamaduni na mtazamo wao kilimwengu kutoka kizazi kimoja hadi chengine.

Kuhifadhi Historia na Utamaduni, Katika kuhifadhi amali muhimu za kijamii, wanajamii watapata kufahamishwa kifasihi simulizi historia yao – wao ni nani na wanachimbukia wapi, maana ujuzi utatoka kwa wazee kuja kwa vijana.

Kuunganisha Vizazi vya Jamii, Fasihi simulizi ni msingi mkubwa wa kuwaunganisha wanajamii waliopo na waliotangulia mbele ya haki. Kwa kutambiwa hadithi, vitendawili, methali na nyimbo zao, umbali wa kiwakati kati ya vizazi vilivyotangulia mbele ya haki, vilivyopo na vijavyo unafupishwa kwa kiasi kikubwa sana.

Mara baada ya kumaliza simulizi tutapata wasaa wa kutembelea moja kati ya Vivutio vyenye historia ya kale sana katika wilaya ya kyela, kivutio hiki ni msitu wa KATAGO.

Kwa watakao penda kushiriki tafadhari piga simu uyole cultural 0766422703, 0783545464 au kyela Enviculture 0783874104

Comments

  1. I'd like to take the power of thanking you for that specialized guidance I've constantly enjoyed viewing your blog.

    check this out

    ReplyDelete

Post a Comment