SAFARI YA KUPANDA KILELE CHA MLIMA WA TATU KWA UREFU TANZANIA. (MLIMA RUNGWE)






Safari ya kupanda Mlima Rungwe wenye sifa madhubuti nchini Tanzania uliratibiwa na Halmashauri ya wilaya ya Rungwe kwa kushirikiana na taasisi mbali mbali kama vile Wildlife conservation society (WCS), African wildlife Foundation (AWF), Mount Rungwe Nature Reserve (MRNR), Tanzania forest services (TFS), Waheshimiwa madiwani wa wilaya ya Rungwe, Kamati ya utalii ya wilaya, Kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya na Uyole cultural tourism enterprises.

Safari hii ilikuwa na jumla ya washiriki Sabini na nne (74) ambao kila mmoja alielezea ni kwa namna gani ameifurahia safari hii, Tulipozungumza na Afisa utalii Dada Levina wa jiji la Mbeya alisema “amefurahishwa sana na mapokeo ya watu juu ya umuhimu utalii wa ndani hivyo anawasihi watu kuendelea kuwa na moyo wa kupenda safari hizi” Lakini pia Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Rungwe pamoja na Afisa mali asili na Afisa utalii wakasema upo mpango madhubuti wa kufanya safari nyingi katika vivutio vya kitalii vipatikanavyo wilaya ya Rungwe ikiwezekana angalau kila mwisho wa mwezi kuwe na safari moja.

MACHO YOOTE YA WADAU WA UTALII KWA SASA YANAELEKEA RUJEWA NA WANGING’OMBE KATIKA SIKU YA KUPATWA KWA JUA. Ukiwa kama mdau wa utalii ndani nan je ya mkoa wa Mbeya tupende kuchukua fursa hii kukukaribisha katika tukio hili kubwa na la kihistoria.

Comments

Post a Comment