Watalii kutoka Zanzibar waliotembelea mkoa wa Mbeya wakiwa wameongozana na baadhi ya viongozi wao akiwemo Mbunge Sarumu Mwinyi Lehani wa jimbo la uzini zanzibar. ugeni huu ni wa watu 160 lakini tulioenda nao kyela walikuwa watu 90 ulipokelewa na Julius Jailo na kisha kutembezwa na Uyole Cultural Tourism Enterprises siku ya jumamosi tar 26/03/2016 wakiwa na coordinator Mwalyego Mwalingo Jr. ambao walitembelea sehemu mbalimbali za mkoa wa Mbeya.
Katika safari hii tulipita wilaya ya Rungwe na wilaya ya Kyela. Wilaya ya Rungwe waliweza kufika Daraja la Mungu Kiwila na baadae kujifunza juu ya kilimo cha chai katika mashamba ya Kyimbila. Lakini katika wilaya ya kyela walitembelea Daraja la kiteputepu (suspension bridge), mpaka wa Tanzania na Malawi (kasumulu) na mwisho ilikuwa bandari ya Itungi (Itungi port) ambapo walishuhudia utengenezwaji wa meli tatu mpya mbili zikiwa za mizigo na moja ikiwa ya abiria.

Comments
Post a Comment