UYOLE CTE TULIPOTEMBELEA CHAI FM RADIO






CHAI FM RADIO 105.7 Inayosikika maeneo mbalimbali ikiwemo Mkoa wa Mbeya na wilaya zake, Mkoa wa Songwe, Njombe na Songea na nchi jirani kama vile Malawi na Zambia. RSTGA inaongozwa na Lebi Gabriel Mtendaji mkuu, na mwenyekiti ni mzee Johnson Mwakasege, Manager ni Kissa Mwamfupe. shukrani za dhati pia kwako Msimamizi wa matangazo na Biashara Ally Kingo

Uyole Cultural Tourism Enterprises, Tupende kutoa shukrani za dhati kwa uongozi wa Chai Fm radio kwa ukarimu, upendo na mapokezi yao, tulifarijika sana kuwa sehemu ya familia ya radio hii, pomgezi za dhati kwa ubunifu wao wa kuwa na kipindi maalum kinachozungumzia utalii na utamaduni. Tulipata wasaa wa kupata elimu mbalimbali kutokana na vitengo mbali mbali vilivyopo mahala pale

Katika safari yetu tulipata wasaa wa wa kufanya nao kipindi na kuona mchango mkubwa wa vyombo vya habari katika kutangaza na kukuza utalii nchini. Pia shukrani za dhati kwa ofisi ya Rungwe Tea and tours kwa ushiriano wao na kwa kazi yao nzuri ifanywayo katika kukuza utalii.

Comments