PANGO LA POPO SONGWE (SONGWE BAT CAVE)

Hili ni pango linalo patikana nje kidogo ya mji mdogo wa Songwe karibu na mto Songwe (Songwe ya Kaskazini) wenye chanzo chake katika milima ya Umalila karibu na Santilya iliyopo kusini ya Mbeya ikielekea kaskazini na kuishia Ziwa la Rukwa. Hukatisha sehemu iitwayo Nanyara juu ipatikanayo kando ya balabala kuu ya TAZAM

Pango hili kama lijulikanavyo kwa jina lake, nisehemu inayotumiwa kama makazi na viumbe wajurikanao kama Popo. Pia ni sehem ya mvuto sana kwa kuitembelea kwa kua imeumbwa kwa muonekano wa aina yake na watofauti kidogo, pango hili ni tofauti na NKYALA RITUAL CAVE lililopo wilayani kyela Mkoani Mbeya.

Pindi utembeapo pango hilo unaweza kuingia kwa kupitia mlango wake ulio kua mdogo kwa kulinganisha na muonekano wake mkubwa uwapo ndani, ambapo unashuriwa kuingia na tochi yenye mwanga mkali ili kuweza kuepuka kutumbukia katika vishimo vidogo vidogo vipatkanavyo ndani ya mapango hayo na kuweza kuivuka kwa uangalifu daraja ndogo linalounganisha pande mbili za pango iliyotengenezwa na binadamu ndani ya pango hili, pia baada ya kuvuka daraja hilo unaweza kupata mwanga kupitia shimo/tundu ambalo hupenya mpaka nje kwa kupita muonekano wa juu wa pango ilo.

Mambo ambayo utaweza kujifunza utembeleapo pango hili na UYOLE CULTURAL TOURISM ENTERPRISES kujua faida nyingi kihistoria ikiwepo matumizi ya pango kabla na baada ya kipidi cha ukoloni, ki jiografia ambapo utajifunza ni jinsi gani mapango hayo yalitokea na yameundwa na miamba ya aina gani na lina urefu gani, pia ya utajiri wa madini gani na kiuchumi ambapo mtembeleaji atajua pango hilo linafaida gani aji wa picha.

Kuna vitu vingi sana ambavyo kwa kupitia safari ya utembeleaji wa pango hilo ataweza kufaidika au kuvipata, mfano; hali ya hewa nzuri ya joto maana uwapo maeneo ya mbeya mjini ni baridi tofauti na ukanda wa mbalizi mpaka songwe, uoto wa asili uliotawaliwa na miombo, kuwaona wanyama wadogo wadogo kama sungura pori (Hare), muonekano mzuri wa safu za milima na mto Songwe, viwanda vya utengenezaji wa vifaa vya ujenzi pamoja kama chokaa, simenti na marumaru, kuujua mji wa songwe na visima vya asili ya maji yamoto

Pia unaweza unaposafiri kuelekea katika pango hilo unaweza kutembelea sehemu kama nyumba ya hifadhi ya makumbusho ya kale (museum) na hifadhi ndogo ya wanyama (zoo) ipatikanayo karibu na Hospitali Teule ya Ifisi maarufu kama kwa Lena, uwanja wa ndege wa kimataifa wa Songwe. Bila kusahau gereza la Songwe. Wasiliana nasi kwa simu 0783545464/0766422703.

Comments