WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII, DKT.DAMAS NDUMBARO ATOA AGIZO KWA TAASISI WIZARA YA MALIASILI NA UTALII KUSHIRIKI TAMASHA LA MAJI MAJI MAJI SELEBUKA
Waziri wa Maliasili na utalii, Dkt. Damas Ndumbaro (kati kati) akiwa na Mkuu wa Wilaya ya Songea, Pololet Mgema (kushoto) na Mratibu Mkuu wa tamasha la Majimaji, Reinafrida Rwezaura (kulia) wakielekea kwenye eneo la kukata utepe kwenye uzinduzi wa tamasha hilo
Waziri wa Maliasili na Utalii ambaye pia ni Mbunge wa Songea Mjini , Dkt. Damas Ndumbaro akikata utepe wakati akizindua rasmi msimu wa saba wa Tamasha la Majimaji Selebuka litakalofanyika kuanzia tarehe 24 hadi 31 Julai kwenye Viwanja vya Maji Maji Songea mkoani Ruvuma. Wa pili kulia ni Mkuu wa wilaya ya Songea, Mhe. Pololet Mgema akiwa na Viongozi wengine wa Kiserikali na Taasisi za Misitu nchini
Waziri wa Maliasili na Utalii ambaye pia ni Mbunge wa Songea Mjini Dkt. Damas Ndumbaro akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa kiserikali na taasisi za misitu pamoja na wageni mara baada ya kuzindua Tamasha la Majimaji Selebuka litakalofanyika kuanzia tarehe 24 hadi 31 Julai kwenye Viwanja vya Maji Maji Songea mkoani Ruvuma.Mratibu Mkuu wa Tamasha la Majimaji Selebuka, Reinafrida Rwezaura akikabidhi risala iliyosomwa kwa Mgeni rasmi Waziri wa Maliasili na na Utalii, Dkt. Damas Ndumbaro
Mkuu wa Wilaya ya Songea, Pololet Mgema akizungumza kabla ya kumbakaribisha Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Damas Ndumbaro kwenye uzinduzi wa Tamasha la Majimaji linalotarajiwa kufanyika kuanzia tarehe 24 hadi 31 Julai 2021
Kikundi cha Ngoma ya Lizombe kikitumbuiza kwenye uzinduzi wa tamasha la Majimaji Selebuka Viwanja vya mashujaa wa vita vya majimaji Mahenge songea
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt.Damas Ndumbaro ameziagiza Taasisi zote za Wizara ya Maliasili na Utalii ambazo zinatangaza Utalii na zinafanya Uhifadhi kuweza kushiriki Tamasha la Majimaji Selebuka.
Tamasha hilo linatarajiwa kufanyika mkoani Ruvuma kuanzia tarehe 24 Julai hadi 31 mwaka huu katika Uwanja wa Majimaji Songea likiwa na lengo la kuhamasisha utalii wa ndani, michezo pamoja na kukuza na kuenzi utamaduni wetu.
Ametoa agizo hilo wakati akizindua msimu wa saba la Tamasha hilo uliofanyika kwa muda wa siku mbili kuanzia 24 na 25 Aprili katika Viwanja vya Makumbusho ya Majimaji ikiwa ni maandalizi ya Tamasha lenyewe litakalofanyika mwezi Julai kwa muda wa siku saba mkoani hapo
Katika Tamasha hilo ambalo kwa mwaka huu limebeba kauli mbiu isemayo " Misitu ni Uchumi " Dkt.Ndumbaro amesema kwa mwaka huu Tamasha linatoa hamasa kwa Jamii kutunza misitu zaidi.
Waziri Dkt. Ndumbaro amesema anategemea Tamasha hilo kwa mwaka huu litakuwa kubwa sana na litatoa fursa kwa Watu mbalimbali kuanza kutembelea vivutio mbalimbali vya Utalii ambavyo vipo mkoani Ruvuma likiwemo Pori la Akiba Lipalamba
Katika hatua nyingine, Amemuomba Mkuu wa Wilaya ya Songea kutumia mamlaka yake ya kuzitaka Taasisi zilizo katika wilaya yake kushiriki katika Tamasha hilo.
'" Mkuu wa wilaya najua una Taasisi nyingi sana katika wilaya yako ninakuomba na ninaamini una Mamlaka hiyo, toa maelekzo kwa Taasisi zote zinanazotoa huduma na kufanya biashara zishiriki Tamasha la Majimaji Selebuka " alisisitiza Waziri Dkt.Ndumbaro
Aidha amezitaka Halmashauri ya Songea pamoja Halmashauri zingine ziweze kushiriki Tamasha hilo
Aidha, Waziri Dkt. Ndumbaro ametumia fursa hiyo kuziomba Taasisi nyingine za Watu binafsi kushiriki katika Tamasha hilo ili ziweze kutoa huduma kwa jamii katika msimu wa Tamasha hilo.
Kwa upande wake Mratibu wa Tamasha hilo Reinfrida Rwezaura, amesema Tamasha hilo tangu kuanzishwa kwake limekuwa ni Jukwaa bora kwa kuwakutanisha Wafanyabiashara, Wajasiliamali, wanamichezo, wanafunzi, na wadau mbalimbali katika kuendelea kuutangaza uchumi na utalii nchini

Comments
Post a Comment