Hifadhi ya Taifa Kitulo ni hifadhi inayopatikana katika ukanda wa Nyanda za juu Kusini Mwa Tanzania, Inapatikana katika mikoa ya Njombe na Mbeya na ina ukubwa wa kilomita za mraba 465.4 kwenye mwinuko wa Mita 2500 – 3000 kutoka usawa wa Bahari.
Uyole cultural tourism enterprise kwa kushirikiania na Busokelo Tv pamoja na Kelvin Jm, Kupitia Programu ya "KARIBU SOUTHERN CIRCUIT" Yenye lengo la Kutangaza Tamaduni na vivutio vya kitalii vinavyopatikana katika Ukanda wa Nyanda za Juu kusini mwa Tanzania tunaamua kupiga kambi ndani ya Hifadhi ya Taifa Kitulo (Kitulo National Park) na kukuletea Picha na masimulizi Mbalimbali kutoka Hifadhini.
Wanyama – Hifadhi ya Taifa Kitulo (Kitulo National Park) ina wanyama mbalimbali wakiwemo Tohe milima, Mbweha, Sungura, Mbega wenye rangi nyeupe na nyeusi, minde, mbuzi mawe pamoja na nyani aliyegunduliwa miaka ya hivi karibuni ajulikanaye kama Rungwecebus Kipunji.
Shirika la kijamii la uhifadhi wanyama pori (Wildlife conservation Society (WCS) Kwa kushirikiana na Shirika la Hifadhi za Taifa (Tanzania National Parks (TANAPA) pamoja na Taasisi ya utafiti wa wanyama pori Tanzania (Tanzania Wildlife Research Institute (TAWIRI) mnamo mwaka 2018 na 2019 walifanikiwa kuwarejesha wanyama waliokuwepo awali kabla eneo hilo halijawa hifadhi, wanyama waliorejeshwa ni Pundamilia na Swala pala (Impala).
Twenzetu tukatalii katika hifadhi ya Taifa Kitulo (Kitulo National Park)
Book Your trip with us.
Email: uyolecte@gmail.com
+255 783 545 464
Follow us on:Twitter
Follow us on: Pinterest
Facebook acc: Uyole Cte
Blog: uyolecte.blogspot.com
Website: www.uyolecultural.com
Click Here to Follow us on Instagram
Facebook page: Uyole Cultural Tourism Enterprises
Things to do in Mbeya | Mbeya tourist atractions | Uyole cultural tourism enterprise
Comments
Post a Comment