Muonekano wa Kilele cha Mlima Rungwe
Wadau wakiwa katika kilele cha Mlima Rungwe
Moja ya Shimo lililotokana na Milipuko ya kivolkeno ambalo huonekana Vizuri unapoelekea katika kilele cha Mlima Rungwe.
Muonekano wa kreta ya Lusiba Lwa misi
Katika picha hii ya kwanza ni Kreta ya Lusiba Lukafu na Mbele Karibu na wingu ni kreta ya Lusiba lwa Misi ambazo zote huonekana kwa uzuri uwapo katika kilele cha Mlima Rungwe
CEO wa Mbeya Boy Brand akiwa Ameshika chupa ya Maji Rungwe
Safari ya kupanda Mlima Rungwe ilihusisha wadau mbalimbali wakiwemo Busokelo Tv, Mazplusfly (Drone masters), Mbeya Boy Brand, Daniel Mlamka,Rehema Charles, Adam Gwankaja, Shamizzle Punchi na kuongozwa na Uyole Cultural Tourism Enterprise (UCTE).
Mlima Rungwe unapatikana Halmashauri ya Wilaya ya Rungwe Mkoani Mbeya, Mlima huu upo ndani ya Hifadhi ya Mazingira ya Asilia Ya Mlima Rungwe unao simamiwa na wakala wa Huduma za Misitu Tanzania.
Tulianza safari yetu Tarehe 22/12/2020 mida ya jioni kundi moja likitokea Kyela na lingine Mbeya Mjini, kisha kufika Syukula ranger post mida ya saa 12:30 jioni na kufanya kambi yetu pale.
Mnamo Tarehe 23/12/2020 ilipofika mida ya 9:30 usiku tukaanza kuamshana na kisha kuanza safari yetu saa 10:00 usiku tukiwa na mwenyeji wetu Mazao Andambike Fungo, mdogo mdogo tukaanza kupanda mlima na kisha kufanya mapumziko njiapanda ya Kuelekea Lusiba.
Bwana weee kulipoanza kupambazuka ndipo kila mmoja alianza kuhamaki na kushangazwa na uzuri wa Mlima huu, kuanzia muonekano wa Milima na Mabonde, misitu iliyozunguka Mlima Huu, lakini pia muonekano wa maeneo mbalimbali ikiwemo Kiwira, Katumba, kandete, Tukuyu, Pamoja na ziwa Nyasa. Mdogo mdogo tukafika katika eneo maarufu kwa jina la mianzini zikapigwa pambio za kumpa nguvu Rehema Charles mpaka tukatoboa katika kilele cha Mlima Rungwe.
Vivutio Vingine Ambavyo mtu anaweza kuona ni Pamoja na.
- Uwepo wa Viumbe Mbalimbali ambao baadhi yao hawapatikani sehemu nyingine yoyote isipokuwa katika Hifadhi ya Mazingira Asilia Mlima Rungwe tu. mfano wa viumbe hao ni nyani aina ya Kipunji (Rungwecebuskipunji) aliyegunduliwa kwa mara ya kwanza katika Hifadhi hii na Shirika la Uhifadhi wa Wanyamapori (WCS) mwaka 2003.
- Urefu wa mita elfu mbili mia tisa themanini na moja (2981) maalum kwa wana mazoezi, na wapanda milima (Mountain Hikers)
- Mashimo ya volkano Kama vile Paluvalalutali, Lusiba Lwamisi, Lusiba Lukafu na Ng’ombe ambayo mashimo hayo kwa sasa yamekufa (Dead volcanic craters).
- Wanyama wadogo wadogo zaidi ya aina miatano (500) kama vile Minde (Abbot duiker), chura wekundu, mijusi, nyoka wa chi baridi na panya
- Ushoroba wa Bujingijila, Ni miongoni mwa eneo muhimu sana kiutalii linalo unganisha Hifadhi ya Taifa ya Kitulo pamoja na Hifadhi ya Mazingira asilia ya Mlima Rungwe, ni eneo ambalo wanyama hupita kutoka hifadhi moja kwenda hifadhi nyingine
- Miti mbalimbali iliyotumika na wazee wetu katika kutibu magonjwa Mbalimbali
Picha zimepigwa na Mazplusfly.
Book Your trip with us.
Email: uyolecte@gmail.com
+255 783 545 464
Follow us on:Twitter
Follow us on: Pinterest
Facebook acc: Uyole Cte
Blog: uyolecte.blogspot.com
Website: www.uyolecultural.com
Click Here to Follow us on Instagram
Facebook page: Uyole Cultural Tourism Enterprises
Email: uyolecte@gmail.com
+255 783 545 464
Follow us on:Twitter
Follow us on: Pinterest
Facebook acc: Uyole Cte
Blog: uyolecte.blogspot.com
Website: www.uyolecultural.com
Click Here to Follow us on Instagram
Facebook page: Uyole Cultural Tourism Enterprises
Things to do in Mbeya | Mbeya tourist atractions | Uyole cultural tourism enterprise
Comments
Post a Comment