
Mnamo siku ya jana 16/11/2016 tuliweza kutembelea wadau mbalimbali wa utalii wa Mkoa wa Iringa, Tuliweza kuwa na mazungumzo ya kina na Hawa (Afisa utalii mkoa wa Iringa) na Kahemela (Afisa Biashara wa mkoa wa Iringa) juu ya namna gani tunaweza kuunganisha nguvu ktk kutunza na kutangaza utalii wa Nyanda za juu kusini mwa Tanzania (Tanzania southern circuit).
Ambapo kwa pamoja tukaadhimia Kuendelea kufanya tafiti za tamaduni na utalii, kuhifadhi, kuendeleza, kutangaza kadri ya uwezo wetu na kuzifanyia biashara rasilimali za utamaduni wetu.
Katika mazungumzo waliweza kuelezea juu ya maonyesho ya kitalii ya Nyanda za juu kusini yanayokwenda kwa jina la KARIBU KUSINI yatakayofanyika kwa mara ya kwanza mkoani Iringa tarehe 27 mpaka 29 mwezi wa 11 na gharama za banda zitakuwa Tsh 150,000/= Hivyo wadau wote mnakaribishwa.
Mara baada ya baada ya kuzungumza na viongozi wa kiserikali tuliweza kutembelea Makumbusho ya Mkoa wa Iringa (Iringa Boma), ambayo inasimamiwa na mradi wa Fahari Yetu (southern Highlands Culture solutions) chini ya project manager Jan Kuever na Jimson S Sanga Assistant Manager tuliweza kuona vitu na historia mbalimbali za Mkoa wa Iringa.
katika makumbusho hii kuna mgawanyiko wa vyumba vitano, Chumba cha 1 Historia ya kabila la wahehe, Chumba cha 2 Tiba asilia, Chumba cha 3 Tamaduni za Iringa, Chumba cha 4 Chumba cha majaribia, Chumba cha 5 Taarifa za mkoa wa Iringa.
Comments
Post a Comment