Chemchemi za Maji moto, Ni Maji yatokayo ardhini yaliyopashwa joto na nishati ya ardhi na kufyonza madini (Magadi na chumvi chumvi) kutoka kwenye miamba iliyoyeyuka, na kububujika yakiwa chemchemi za maji ya moto. Maji moto Kilambo ni moja kati ya chemchemi za maji moto zinazopatikana Mkoani Mbeya, Chemchemi hii inapatikana Wilaya ya Rungwe halmashauri ya Busokelo.
Sehemu hii ina chemchemi tofauti tofauti tano (5) ambazo ziko mbalimbali kidogo, kwa mujibu wa wenyeji wanasema chemchemi ya mwisho ndiyo yenye chumvi chumvi kuliko hizi zingine inasemekana ukifuata ukanda huo huo unaungana maji moto ya Kyela
BESENI LA TIBA, Ipo sehemu maalum yenye muonekano wa Swimming pool wenyeji wanaiita Beseni la Tiba si kubwa sana na maji yake ni ya uvugu vugu ambayo kwa mujibu wa wenyeji wetu wanasema wao pamoja na wageni hupatumia kama sehemu ya tiba kwa watu wenye matatizo ya Ngozi, wanasema ukiwa na Vipele, Mapunye, Harara, vidonda na magonjwa mengine ya Ngozi unaponywa kabisa baada ya kuyatumia kwa kuoga mara kadhaa, wakaongeza kwamba mtu kama anajisikia homa ama uchovu akiyaoga anaimarika kiafya.
Lakini pia katika moja ya chechemi kuna sehemu maalum ambayo limewekwa kabisa hadi jiwe la kukalia na ina maji ya moto kidogo kuliko ile ya kwanza ambayo hutumika hasa kujikanda sehemu mbali mbali ambazo mtu huweza kuwa na maumivi hasa ya mifupa, vidonda na majeraha.
Maji haya pia yana faida zingine hasa kwa wanyama, miaka iliyopita ilitumika sana na watu wa kutoka maeneo mbali mbali kama Ukinga, Lufilyo, Itete, Lwangwa na maeneo mengine kuja kunywesha mifugo yao, ni sehemu ambayo ina madini ya magadi yenye chumvi chumvi ambayo ni muhimu sana kwa wanyama kiafya.
Ni moja kati ya sehemu ambazyo hupaswi kuzikosa pindi utembeleapo Mkoa wa Mbeya
Best regards Chai Fm radio, Kingo super production and East Africa radio.

Phone: 0756929868/ 0625747086
Email: uyolecte@gmail.com
instagram: uyoleculturaltourismenterprise
Facebook page: Uyole Cultural Tourism Enterprises
Facebook acc: Uyole Cte
Blog: uyolecte.blogspot.com
Visit our office Located at Uyole ya Kati Mbeya.
Email: uyolecte@gmail.com
instagram: uyoleculturaltourismenterprise
Facebook page: Uyole Cultural Tourism Enterprises
Facebook acc: Uyole Cte
Blog: uyolecte.blogspot.com
Visit our office Located at Uyole ya Kati Mbeya.
Best regards Chai Fm radio, Kingo super production and East Africa radio.
Comments
Post a Comment