Daraja la Kamba linaloelea (Kiteputepu) Linalopatikana Mkoani Mbeya katika Wilaya ya Kyela. linapatikana katika mto Kiwira wenye chanzo chake huko wilayani Rungwe na kisha kumwaga maji yake Ziwa Nyasa. Daraja hili ni kiungo muhimu kinachounganisha kata za ndandalo na ikimba, Wilaya ya kyela ina madaraja mengine ya Kamba ambayo ni kasumulu, lema na ipande.
Madaraja matatu (3) yapo katika mto kiwira ambayo ni ndandalo, kasumulu na lema na daraja moja lipo katika mto mbaka ambalo ni Ipande, Uwapo wilayani humu utaweza kujifunza na kushiriki katika shughuri mbalimbali ikiwemo kilimo cha kokoa, michikichi, mpunga, migomba na NK lakini pia unaweza kutizama ngoma za asili za Wanyakyusa, kujifunza namna biashara zinavyofanyika katika mpaka wa Tanzania na Malawi. Shukrani za dhati kwa mkurugenzi Mtendaji wa wilaya ya Kyela CR. KASONGO na Mhifadhi J. MBAGA. Karibu Tanzania, Karibu Mbeya, Karibu kyela.
Comments
Post a Comment