Ngosi ni ziwa la kreta (crater lake) lipatikanalo Mkoa wa Mbeya kwenye milima ya Uporoto, Wilaya ya Rungwe lipo katika nyuzi 9.008°Kusini na 33.553°Mashariki, ni ziwa la pili kwa ukubwa barani Afrika katika crater lake baada ya lile lililoko nchini Ethiopia.
Hata hivyo, wataalamu wanasema kwamba Ziwa Ngosi lina sifa za kipekee linazolitofautisha na lile lililoko Ethiopia. Moja ya tofauti hizo ni kwamba Ziwa Ngosi limezungukwa na milima na misitu minene tofauti na lile la Ethiopia ambalo liko eneo lililo wazi na hufikika kwa urahisi kabisa kwa gari kitu ambacho hakiwezekani kwa Ziwa Ngosi.
Wataalamu wanasema kwamba kuwepo kwa ziwa hilo sehemu hiyo kunasaidia kuzuia milipuko ya mara kwa mara ya volkano kwa kuwa linasaidia kupunguza misukumo ya gesi inayojijenga chini na kuanza kutafuta upenyo wa kutokea chini ya ziwa.
Kitu cha kushangaza ni muonekano wa ziwa hili linakaribia kuwa na muonekano kama ramani ya bara la afrika pamoja na visiwa vyake kama ilivyo kule njombe ambapo kuna mwamba wenye ramani ya bara la
Afrika unaitwa Lwivala, uliopo katika pori la hifadhi ya msitu Lwivala kijiji cha Igodivaha. Wilaya ya Njombe ziwa hili pia lina ingiza tu maji na hali toi maji kwa sababu liko katikati ya milima hivyo kuonekana kama liko shimoni alafu halina ufukwe.

Ziwa hili linalopatikana katika Hifadhi ya msitu Uporoto (Poroto Ridge) yenye eneo la hekta 9,332 ipatikanayo karibu na vijiji vya Kisanga 4.3km Uyole (24.4km) na mji mdogo wa Tukuyu upatikanayo wilaya ya Rugwe.
Zipo imani nyingi juu ya ziwa hilo la maajabu watu husema ziwa hili lilichomwa moto na wakazi wa kijiji cha Mwakaleli kwasababu lilikuwa likileta mikosi mingi kijijini hapo ikiwemo vifo vya mara kwa mara kwa watu na wanyama, kitaalam ziwa haliwezi kuhama kutoka sehemu moja kwenda nyingine, Zipo imani miongoni mwa watu kuwa ziwa ngosi watu wanapotea kimazingara.
kuwapo kwa sauti za watu wasioonekana ndani ya misitu, wengine huamini huruhusiwi kuzungumza kinyakyusa, huruhusiwi kunywa maji wengine husema ziwa hilo limekuwa likigeuka rangi mara kwa mara na kuwa na rangi za kijani, bluu,
nyeusi na nyeupe kitu ambacho kinawafanya waamini kuwa ziwa hilo sio la kawaida.(tulikunywa maji pia tulizungumza kinyakyusa mpaka leo hatujaudhurika)
nyeusi na nyeupe kitu ambacho kinawafanya waamini kuwa ziwa hilo sio la kawaida.(tulikunywa maji pia tulizungumza kinyakyusa mpaka leo hatujaudhurika)
Chief mkuu wa wasafwa mkoa wa mbeya Chifu Rocket Masoko Mwanshinga alisema ni jambo la
ajabu na kusikitisha sana kuona ziwa ngosi linafahamika sana kwa wageni kuliko wenyeji, hivyo anapenda kutoa wito kwa wadau wote wa utalii kulitangaza ziwa hili ili liweze kufahamika sana ndani na nje ya nchi.

Alisema jina ZIWA NGOSI ni la kisafwa linalotokana na neno GOSI lenye maana ya kubwa hivyo kwa wasafwa walimaanisha ziwa kubwa na pia alisema maji ya ziwa lile ni maji safi na ya yenye baraka tofauti na vile watu wanaamini
Kuna baadhi ya vitu ambavyo vinakwamisha sana kukua ama kufahamika kwa ziwa ngosi miongoni mwa vitu hivyo ni pamoja na, Miundo
mbinu mibovu ambayo hupelekea watalii kushindwa kufika kwa urahisi katika eneo husika, Viongozi wachache wa safari (tour guides) Matangazo ya kivutio, Taarifa na maelezo hafifu ya kivutio, Makosa ya matamshi ya jina.

Pamoja na hayo Jitihada muhimu zinahitajika ikiwemo kuzuia mmomonyoko wa udongo unaosababisha udongo kuingia ziwani hivyo kupunguza kina cha ziwa, kujenga angalau ngazi zenye sehemu za kujishikiria katika baadhi ya maeneo ambayo ni tatanishi/magumu kupanda ama kushuka, vyombo mbali mbali vya habari kujitokeza kwa wingi kulitangaza ziwa ngosi, pia kujenga kijisehemu kidogo ambacho kitatoa huduma
muhimu ikiwemo chakula na vinywaji.
muhimu ikiwemo chakula na vinywaji.
Kwa safari (tour)/maelezo/masimulizi/habari za kitalii na utamaduni wasiliana nasi UYOLE CULTURAL TOURISM ENTERPRISES.
0783545464/0766422703
0783545464/0766422703
Comments
Post a Comment