ziwa hili lipo eneo liitwalo lugombo katika kijiji cha kabembe kata ya itete umbali mdogo kutoka hospitali teule ya Itete, na uwapo juu hospitalini unaweza kuona kwa uzuri ziwa kiungululu na ziwa nyasa.
Katika ziwa hili Hakuna mto wowote unaoingiza wala kutoa maji na ajabu yake nyingine ni kwamba wakati wa masika maji hupungua na wakati wa kifuku huongezeka.
Ziwa hili lina samaki kiasi wakubwa kwa wadogo, uwapo kiungululu ukitizama kwa mbali utaona safu zenye kupendeza za milima livingstone iliyoambaa pembezoni mpaka katika kingo za ziwa nyasa.
Katika masimulizi ya kihistoria juu ya utokeaji wa ziwa kiungululu tulipozungumza na chief wa eneo lile Chief Angulile Mbonile Mwangake, pamoja na wazee wengine kila mmoja alisimulia kwa namna yake lakini walilenga kitu kimoja.
kulikuwa na mtu mmoja alitoka sehemu za mbali sana na kufika mahali hapa, alipofika alionekana kuwa ovyo sana kwa maana ya kwamba alikuwa mchovu na mchafu sana mithiri ya mtu aliyegalagazwa katika vumbi, aliingia katika nyumba ya kwanza ili kuomba maji ya kunywa kutokana na hali aliyokuwa nayo ya uchafu walimkatalia, basi akasogea katika nyumba ya pili vivyo hivyo wakamkatalia na kumfukuza.
Alipofika katika nyumba ya tatu alimkuta mama mmoja msamalia mwema ambae alimuonea huruma kwa hali aliyokuwa nayo na kumkirimu kwa kumpa maji ya kuoga, akamvisha nguo zingine na kisha kumwandalia chakula, mara baada ya kumaliza kula ndipo yule mtu akamwambia mama yule uhame mahala hapa uhamie sehemu nyingine kwa maana hapa patatokea maajabu, wale watu walipomwona
mama yule anahama wakamsema na kumtukana kwa kusema kichaa anamhamisha na kumuona
kama mtu asiekuwa na akili kabisa, baada ya kutii agizo lile ikawa kama pigo kwa wale watu waliokuwa wamebaki pahala pale Pakadidimia na kisha yakaibuka maji.
Masimulizi hayo yalitumika ili kutoa elimu kizazi hata kizazi kuzifanya jamii kuwa na ukarimu na upendo maana masimulizi hayo hayo yalitumika hata katika maeneo mengine mfano kisiba, ikapu, ilamba na kingili.
lakini kijiografia inasemekana ziwa kiungululu lilitokana na mlipuko wa kivolkano iliyotokea miaka mingi iliyopita mfano wa maziwa mengine ni ziwa ngozi, kisiba n.k.
Kwa safari za kitalii/ habari za utalii na utamaduni katika jiji la Mbeya karibu UYOLE CULTURAL TOURISM ENTETPRISES.
Karibu mbeya, karibu busokelo, karibu Rungwe, karibu uyole cte.
Sijawahi kulijua hili ziwa hapo kabla nimepata furaha zaidi kuliko nilivyolijua ziwa Ngozi. Nimevutiwa sana na natamani nifike niliona vizuri.
ReplyDeleteKaribu sana tena sana, we will take you there
DeleteUtafiti ufanyike wa kutosha maana nasikia ziwa halitumiwi katika shughul zozote km kufua nguo kupikia na uvuvi
ReplyDeleteUwezo Mwasilembo
ReplyDelete