ASILI YA NENO TUKUYU.

Tukuyu Ni mji upatikanao kilomita 70 kutoka jiji la mbeya pia kilomita 53 kutoka kyela, hivyo kufanya jumla ya kilomita 123 mbeya mpaka kituo cha mabasi kyela, Tukuyu ni Makao Makuu ya Wilaya ya Rungwe katika Mkoa wa Mbeya.

Ni moja ya maeneo yanayokaliwa na watu wa kabila la Wanyakyusa na ni Kabira ambalo linafahamika vyema kwa kilimo cha ndizi, chai, kahawa, maharage, mahindi, magimbi, viazi vitam na mvilingo na ufugaji wa mifugo mbalimbali na kadhalika.

Mji wa tukuyu ni mji wenye hali ya hewa safi na ubaridi baridi kwa kipindi kikubwa cha mwaka, eneo hili hupokea mvua kwa kiwango kikubwa sana katika kipindi cha masika na kwa sehemu kubwa zaidi ya mwaka.

Tukuyu ilianzishwa wakati wa ukoloni wa Kijerumani ikaitwa Neu Langenburg
("boma ndefu mpya") badala ya Langenburg ya awali iliyokaa mwambaoni wa Ziwa Nyasa ikazama chini wakati wa maji ya ziwa kupanda. Hadi leo jina la hoteli kuna hoteli iitwayo "Langiboss" inakumbuka jina la zamani.

je asili ya mji huo kuitwa Tukuyu ni ipi? Eneo ambalo leo uko mji wa Tukuyu lilikuwa na miti aina ya mikuyu. Hivyo wenyeji wa sehemu hiyo ambao ni Wanyakyusa, wakawa wanapaita mahali hapo ‘patukuju’ yaani mahali penye miti ya mikuyu.

Kutokana na lafudhi ya Wanyakyusa, kwao ilikuwa rahisi kusema ‘tukuju’ badala ya ‘tukuyu’!” Katika mwingiliano wa makabila mengi yaliyokuwa eneo hilo, wakiwemo wakoloni ambao walikuwa na majukumu ya kuweka kumbukumbu mbalimbali za maeneo nchini, neno ‘tukuju’ likabadilika na kuwa ‘tukuyu’ na hivyo kuwa jina la mji huo ulio kusini mwa Jiji la Mbeya katika barabara kuu iendayo mji wa Kyela ulio kando ya Ziwa Nyasa na nchi ya Malawi. Na mikuyu ambayo ndiyo chanzo cha jina la Tukuju/Tukuyu ilikuwa ipo bomani kwenye tank ya maji ambalo linasambaza maji karibu mji wote wa Tukuyu na mpaka sasa ipo michache karibu na tank jipya la chini.

Hapo bomani ilikuwa ngome ya kivita ya wajerumani na ndio mwanzo wa jina la boma na kirefu chake ni Base of Military Administration (BoMA) na hadi leo hayo majengo bado yapo, na kuna vidirisha ambavyo ndani ni vikubwa na kwa nje vidogo iliwasaidia wajerumani kumwona adui kirahisi na adui kupata shida kuona kutoka nje.

Mji huu umejengwa kwa juu kama ktk mlima hivi hata tank la chuma lililojengwa na wajerumani liliwekwa hapo kurahisisha usambazaji maji kwa chini kwasababu mitaa yooote ya kamji haka kazuri ipo kama kwenye miteremko hivi na ndilo mpaka leo linatumika, na lipo juu katika kilele cha mji huu.


Nadharia juu ya asili, utokeaji au historia ya kitu fulani huwa zinakuwa nyingi kidogo hii ni moja ya nadharia nliyokumbana nayo, usisite kucomment ile wewe uijuayo ili watu waweze kuifahamu.

Kwa safari/maelezo/habari za utalii na utamaduni katika mkoa wa mbeya fika UYOLE CULTURAL TOURISM ENTERPRISES.

Comments